• Contact us |
    • FAQ |
    • Complaints |
    • Gms |
SHIRIKA LA MASOKO YA KARIAKOO
SHIRIKA LA MASOKO YA KARIAKOO

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania OFISI YA RAIS TAWALA ZA MIKOA NA SERIKALI ZA MITAA SHIRIKA LA MASOKO YA KARIAKOO

  • Home
  • About KMC
    • Vision and Mission
    • Organization Structure
    • Core Functions
  • Adminstration
    • Departments
      • Human Resources and Administration
      • Health and Sanitation
      • Finance
      • Planning and Commercial
    • Units
      • Maintenance Service
      • Internal Audit
      • Procurement Management
      • Information and Communication Technologies
      • Legal Services
      • Security
  • Media Center
    • News
    • Announcements
    • Gallery
    • Press-Releases
    • Videos
  • Marketing
    • Products and Services
    • Marketing Price
  • Investment and Projects
    • Ongoing Projects
    • Completed Projects
    • Upcoming Projects
    • Investment Opportunities
  • Procurement
    • Tenders
  • Publications
    • Guidelines
    • Forms
    • Journals/Newsletter
    • Reports
    • Speeches
  • E- Services Links
    • Revenue Collection(TAUSI)
    • GISP Portal
    • Employees Self Service Portal
    • E - Mrejesho
    • E - Board
    • E - Mikutano

Soko La Kariakoo Kuanza Rasmi Februari 2025

Posted on:: May 13th, 2025

JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA 

                                       OFISI YA RAIS



 

TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI

Dar es Salaam, 29 Januari,2025

Ndugu wanahabari

Nimewaita hapa leo kuzungumza nanyi juu ya hatua zinazoendelea kwenye maandalizi ya kurejesha shughuli za biashara kwenye soko la Kariakoo. Itakumbukwa kuwa soko la Kariakoo lilipata ajali ya moto tarehe 10 Julai 2021 na kusababisha wafanyabiashara kuondolewa na shughuli kusimama.

Tangu kipindi hicho serikali ya Awamu ya Sita inayoongozwa na Mheshimiwa Dkt. Samia Suluhu Hassan, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania imekuwa ikitekeleza mradi wa ujenzi na ukarabati wa soko hilo ulioanza mwezi Januari 2022 na sasa umefikia hatua za kukamilika. Tunamshukuru Mheshimiwa Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan kwa kutoa fedha kiasi cha shilingi Bilioni 28.03 zilizotumika kufanikisha mradi huu wa kimmkakati wenye nia ya kulifanya Soko la Kariakoo kuwa la kimataifa.

Ndugu wanahabari

Tarehe 27 Januari 2025 Bodi ya Wakurugenzi ya Shirika ilikutana hapa Dar es Salaam ambapo pamoja na agenda zingine ilijadili na kuazimia kuwa kazi ya kuwarejesha wafanyabiashara kwenye soko la Kariakoo ianze mapema mwezi Februari mwaka huu. Uamuzi huu wa Bodi ya Wakurugenzi unafuatia kukamilika kwa ujenzi na ukarabati wa soko sambamba na kukamilika kwa kazi ya uhakiki wa waliokuwa wafanyabiashara kwenye soko hilo uliofanywa na Timu Maalum iliyoundwa na Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam ikijumuisha wawakilishi  wa Wafanyabiashara, Menejimenti ya Shirika la Masoko ya Kariakoo na vyomba vya Usalama.

Kwa niaba ya Bodi ya Wakurugenzi wa Shirika ninachukua fursa hii kuwajulisha wananchi na wafanyabiashara kuwa Soko la Kariakoo litarejesha shughuli zake kuanzia mwezi Februari, 2025. Menejimenti inaratibu kazi ya kutangaza majina ya waliokuwa wafanyabiashara kwenye Soko hilo ambao wamekidhi vigezo na sifa za kurejeshwa baada ya uhakiki. Uhakiki uliofanywa umebaini jumla ya wafanyabiashara1,520 wanaotarajiwa kurejeshwa sokoni. Majina na fomu ya kujiunga vitatangazwa kwa umma kupitia  vyombo vya habari ikiwemo tovuti ya Shirika la Masoko ya Kariakoo na tovuti ya OR - TAMISEMI.

Hivyo nitoe wito kwa wafanyabiashara na wananchi kuwa Shirika la Masoko ya Kariakoo kwa kushirikiana na mamlaka zingine za Serikali ikiwemo Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam itaendelea kutoa taarifa kwa wananchi juu ya utaratibu utakaotumika kipindi chote cha kuelekea ufunguzi wa soko la Kariakoo.

Ndugu wanahabari

Natoa wito kwa Wafanyabiashara wote wenye madeni kulipa madeni yao kabla ya kurejea Sokoni. Takwimu zetu zinaonyesha jumla ya wafanyabiashara 366 wanadaiwa na Shirika Shilingi 358,571,106.85.

Wafanyabiashara na wananchi wote wenye sifa za kuingia sokoni watatangaziwa utaratibu utakaotumika, hivyo Shirika linawataka kuendelea kuwa na subira wakati Mamlaka zikikamilisha taratibu. 


Asanteni kwa kunisikiliza.

Hawa Abdurahman Ghasia

MWENYEKITI WA BODI YA WAKURUGENZI

 

S.L.P 15789, DAR ES SALAAM

Barua-pepe  : info@kariakoomarket.co.tz   Tovuti : www.kariakoomarket.co.tz 

Announcements

  • Taarifa kwa Umma January 31, 2025
  • Taarifa kwa Umma January 29, 2025
  • Usajili wa wafanyabiashara November 14, 2023
  • Tangazo la Uchaguzi wa Serikali za Mitaa 2024 August 15, 2024
  • View All

Latest News

  • Mafunzo ya Afya kwa Watumishi Soko la Kariakoo

    May 10, 2025
  • Mei Mosi 2025

    April 30, 2025
  • Wastaafu Soko la Kariakoo Kulipwa Milioni 306

    April 18, 2025
  • Wabunge Wapongeza Serikali Mradi wa Soko la Kariakoo

    April 13, 2025
  • View All

Video

More Videos

Quick Links

  • TAMISEMI
  • eGovernment Authority
  • Employees Self Service Portal

Related Links

World visitors tracker

world map hits counter

Contact us

    General Manager, Kariakoo Markets Corporation, Nyamwezi/Tandamti Street,

    Postal Address: P. O. Box 15789 Dar es Salaam, Tanzania

    Telephone: +255 22 2180678

    Mobile:

    Email: info@kariakoomarket.co.tz

Other Contacts

   

Visitors Counter

www.freevisitorcounters.com

    • FAQ
    • Privacy Policy
    • Disclaimer
    • Sitemap
    • Service

Copyright ©2024 Shirika la Masoko ya Kariakoo . All rights reserved.