Shughuli za biashara katika Soko la Kariakoo zitaanza tena rasmi mwezi Februari mwaka huu 2025 baada ya kukamilika kwa kazi ya uhakiki wa waliokuwa wafanyabiashara kwe ye soko hilo kabla ya ajali ya moto ya Julai 10 mwaka 2021.
Akizungumza kwa niaba ya Bodi ya Wakurugenzi wa Shirika hilo, Mwenyekiti wa Bodi hiyo Mheshimiwa Hawa Ghasia alisema Soko la Kariakoo litarejesha shughuli zake kuanzia mwezi Februari, 2025 ambapo kwa sasa Menejimenti inaratibu kazi ya kutangaza majina ya waliokuwa wafanyabiashara kwenye Soko hilo ambao wamekidhi vigezo na sifa za kurejeshwa baada ya uhakiki.
"Uhakiki uliofanywa umebaini jumla ya wafanyabiashara1,520 wanaotarajiwa kurejeshwa sokoni" alisema Ghasia wakati akiongea na waandishi wa habari Januari 29 mwaka huu jijini Dae es Salaam.
Mwenyekiti huyo aliongeza kusema majina na fomu ya kujiunga vitatangazwa kwa umma kupitia vyombo vya habari ikiwemo tovuti ya Shirika la Masoko ya Kariakoo na tovuti ya OR - TAMISEMImwishoni mwa wiki hivyo wananchi wote wawe na subira kuona majina yao.
Katika hatua nyingine Mhe.Ghasia alitoa wito kwa wote wanaodaiwa kulipa madeni yao kabla ya kurejea sokoni ambapo alisema jumla ya wafanyabiashara 366 waliokuwepo sokoni kabla ya ajali ya moto wanandaiwa kiasi cha shilingi Milioni 358.5
General Manager, Kariakoo Markets Corporation, Nyamwezi/Tandamti Street,
Postal Address: P. O. Box 15789 Dar es Salaam, Tanzania
Telephone: +255 22 2180678
Mobile:
Email: info@kariakoomarket.co.tz
Copyright ©2024 Shirika la Masoko ya Kariakoo . All rights reserved.