Shirika la Masoko ya Kariakoo limesaini mkataba wa makubaliano na Shirika la Bima la Taifa kwa ajili ya menejimenti ya vihatarishi vitakavyoweza kutokea katika soko jipya la Kariakoo hatua itakayosaidia kupata fidia ya hasara.
Mkataba huo wa makubaliano ya utoaji huduma za bima kwa Soko jipya la Kariakoo umesainiwa baina ya Meneja Mkuu wa Shirika la Masoko ya Kariakoo CPA Ashraph Abdulkarim na Mkurugenzi Mtendaji wa Shirika la Bima la Taifa Kaimu Abdi Mkeyenge leo (Jumatano (30 Julai 2025) jijini Dar es Salaam.
Akieleza lengo la mkataba huo CPA Abdulkarim alisema Serikali ya Awamu ya Sita imewekeza zaidi ya shilingi Bilioni 28 kujenga na kukarabati soko baada ya ajali ya moto ya 10 Julai 2021 hivyo ni budi kulinda miundombinu hiyo kwa kukata bima.
CPA Abdulkarim aliongeza kusema uamuzi huo umelenga kulinda mali za umma na kwamba wafanyabiashara watakaoingia ndani ya soko jipya la Kariakoo pia wataelimishwa kupata huduma za bima ili kukinga na majanga.
Kwa upande wake Mkurugenzi Mtendaji wa Shirika la Bima la Taifa Kaimu Abdi Mkenyenge alisema Shirika hilo ni kampuni ya Serikali yenye jukumu la kutoa huduma bora za bima hivyo uamuzi wa Soko la Kariakoo kuwa na bima umekuja wakati sahihi.
Mkeyenge aliongeza kusema, Shirika lake litatoa huduma bora za bima kwa Taasisi zote za umma na binafsi ili majanga yakitokea waweze kurudishiwa hasara itakayokuwa imetokea.
Mkurugenzi huyo alitoa wito kwa taasisi zingine zilizopo chini ya Ofisi ya Rais TAMISEMI ikiwemo halmashauri nchini zenye majengo ya masoko kupata huduma za bima ili kuepusha hasara pale matukio ya vihatarishi ikiwemo moto yatakapotokea.
Shirika la Masoko ya Kariakoo lipo kwenye maandalizi ya ufunguzi wa soko baada ya kukamilika kwa mradi wa ujenzi na ukarabati ambapo wafanyabiashara watarejeshwa kuendelea na biashara.
Mwisho
General Manager, Kariakoo Markets Corporation, Nyamwezi/Tandamti Street,
Postal Address: P. O. Box 15789 Dar es Salaam, Tanzania
Telephone: +255 22 2180678
Mobile:
Email: info@kariakoomarket.co.tz
Copyright ©2024 Shirika la Masoko ya Kariakoo . All rights reserved.