KARIAKOO, URA SECURITY KUIMARISHA ULINZI SOKO LA KARIAKOO.
Meneja Mkuu wa Shirika la Masoko ya Kariakoo CPA. Ashraph Abdulkarim amekutana na kufanya mazungumzo na uongozi wa Shirika la Uzalishaji Mali la Jeshi la Polisi kupitia kampuni yake ya Ulinzi ya URA Security ambayo ndiyo yenye dhamna ya ulinzi wa Soko la Kariakoo.
Mazungumzo hayo yamejikita katika kuweka mikakati ya kuboresha shughuli za ulinzi na usalama wa raia wanaoingia sokoni hapo pamoja mali za wadau mbalimbali wanaotumia soko hilo kongwe na kubwa katika ukanda wa Afrika Mashariki na Kati.
CPA. Abdulkarim ameutaka uongozi wa kampuni hiyo kuendelea kuzingatia utu, lugha nzuri na heshima wakati wa utekelezaji wa majukumu yao kwa kuwa soko hilo linapokea watu mbalimbali na wenye haiba tofauti.
“Kila mtu anao wajibu wa kufurahia huduma nzuri tunazotoa kwa wateja wetu huku tukizingatia kila anayeingia anakuwa salama yeye pamoja na mali zake wakati wote, hivyo tuendelee kuhakikisha tunasimia misingi ya kazi zetu na tunazifanya kwa weledi mkubwa” ameongeza CPA. Abdulkarim
Akiongea kwa niaba ya Mtendaji Mkuu wa Shirika la Uzalishaji Mali la Jeshi la Polisi, Bw. Shukuru Makaranga amelihakikishia Shirika la Masoko ya Kariakoo kuwa wakati wote watatoa huduma nzuri kwa kuzingatia weledi, nidhamu na mifumo sahihi ya mawasiliano iliyopo ili kuhakikisha changamoto zote zinashughulikiwa kwa wakati.
Copyright ©2024 Shirika la Masoko ya Kariakoo . All rights reserved.