KARIAKOO YAJA NA MWAROBAINI WA MAEGESHO, MAGARI ZAIDI YA 400 YAEGESHWA KWA SIKU.
Wananchi wa mkoa wa Dar es Salaam na maeneo ya jirani wamefurahishwa na uwepo wa maegesho yaliyopo Soko Kuu la Kariakoo ambayo yana uwezo wa kuchukua magari zaidi 400 kwa wakati mmoja huku magari zaidi ya 1000 yakikadiriwa kuingia na kutoka katika maegesho hayo.
Wananchi hao wameeleza kuwa kabla ya kuwepo maegesho hayo walikuwa wanahangaika kutafuta maeneo ambayo wanaweza kuegesha magari hayo, huku ikiwachukua zaidi ya nusu saa bila mafanikio kitu kilichokuwa kikiwafanya kutotumia magari yao binafsi wanapoenda Kariakoo kwa ajili ya kupata mahitaji mbalimbali.
“Maegesho ya magari kwa eneo la Kariakoo ni changamoto sana lakini tunaishukuru Serikali kujenga maeneo ya kuegesha magari katika Soko Kuu la Kariakoo, hii imetatua changamoto nyingi sana, magari yanapaki maeneo yenye kivuli na usalama wa kutosha, tusisite kuja na magari yetu Kariakoo” ameshuhudia Bw. Kassim mkazi wa Kimara
Akielezea maegesho hayo, Meneja Mkuu wa Shirika la Masoko ya Kariakoo, CPA. Ashraph Abdulkarim amesema uwepo wa maegesho ya magari ndani ya Soko la Kariakoo kumerahisisha utoaji wa huduma kwani hapo awali mtu alilazimika kuegesha gari lake eneo tofauti na kwenda kwenye soko hilo na wakati mwingine inaleta usumbufu hasa wanapokuwa na mizigo.
“Kipekee namshukuru Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan kwa kukarabati na kujenga jengo jingine jipya katika Soko letu la Kariakoo ambapo ujenzi na ukarati huo kumehusisha pia ujenzi wa maegeshi ya magari ambayo yameleta tija kubwa sana kwa wakazi wa mkoa wa Dar es Salaam na maeneo ya jirani” amebainisha CPA. Abdulkarim.
Copyright ©2024 Shirika la Masoko ya Kariakoo . All rights reserved.