• Wasiliana nasi |
    • Maswali ya Mara kwa Mara |
    • Complaints |
    • Gms |
SHIRIKA LA MASOKO YA KARIAKOO
SHIRIKA LA MASOKO YA KARIAKOO

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania OFISI YA RAIS TAWALA ZA MIKOA NA SERIKALI ZA MITAA SHIRIKA LA MASOKO YA KARIAKOO

  • Mwanzo
  • Kuhusu sisi
    • Dira na Dhima
    • Muundo wa Taasisi
    • Majukumu ya msingi
  • Utawala
    • Idara
      • Human Resources and Administration
      • Health and Sanitation
      • Finance
      • Planning and Commercial
    • Vitengo
      • Maintenance Service
      • Internal Audit
      • Procurement Management
      • Information and Communication Technologies
      • Legal Services
      • Security
  • Kituo cha habari
    • Habari
    • Matangazo
    • Maktaba ya picha
    • Press-Releases
    • Video
  • Marketing
    • Products and Services
    • Marketing Price
  • Miradi na Fursa za uwekezaji
    • Miradi iliyokamilika
    • Miradi inayoendelea
    • Miradi itakayotekelezwa
    • Fursa za Uwekezaji
  • Manunuzi
    • Zabuni
  • Machapisho
    • Miongozo
    • Fomu
    • Journals/Newsletter
    • Reports
    • Hotuba
  • Huduma mtandao
    • Revenue Collection(TAUSI)
    • GISP Portal
    • Employees Self Service Portal
    • E - Mrejesho
    • E - Board
    • E - Mikutano

RAIS SAMIA AWAPUNGUZIA KODI WAFANYABIASHARA SOKO KUU LA KARIAKOO.

Posted on: March 9th, 2026

RAIS SAMIA AWAPUNGUZIA KODI WAFANYABIASHARA SOKO KUU LA KARIAKOO.

 

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan ametoa punguzo la kodi kwa wafanyabiashara wa Soko Kuu la Kariakoo ambapo kwa wafanyabiashara wa vizimba wamepata punguzo la asilimia 17 huku wale wa biashara zingine kama maduka wamepata punguzo la asilimia 10 hadi 16.


Uamuzi huo wa Rais Samia umetangazwa kwa waandishi wa habari na Meneja Mkuu wa Shirika la Masoko ya Kariakoo CPA. Ashraph Abdulkarim ambapo ameongeza kuwa pamoja na punguzo hilo la kodi Mhe. Rais ametoa msamaha wa kodi ya mwezi mmoja tangu alipofungua soko hilo Februari 8,2026 hadi Machi 8, 2026.


“Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Samia Suuhu Hassan ameridhia punguzo hilo la kodi kutokana na maombi ya wafanyabiashara waliyoyatoa kwake kutokana na changamoto mbalimbali walizokumbana nazo baada ya soko hili kupata ajali ya moto mwaka 2021, hivyo tunamshukuru Mhe. Rais kwa moyo wake wa usikivu na upendo mkubwa kwa wafanyabiashara” ameongeza CPA. Abdulkarim


Kabla ya kukutana na waandishi wa habari alifanya kikao na viongozi wa wafanyabiashara wa soko hilo ili kuwaeleza uamuazi wa Mhe. Rais ambapo walishukuru kwa uamuzi huo ambao umejali utu na kuwapa hamasa ya kuendelea kufanya biashara na kulipa kodi kwa maendeleo ya taifa.


Kwa upande wake Mwenyekiti wa wafanyabiashara sokoni hapo, Bw. Ramadhani Kakandilo ameishukuru Serikali kwa kuwajali wafanyabiashara na kuongeza kuwa wataendelea kushirikiana na uongozi wa soko hilo ili mtaji uliowekwa na serikali uwe na manufaa kwa vizazi vya sasa na vijavyo.


Matangazo

  • Taarifa kwa Umma January 31, 2025
  • Taarifa kwa Umma January 29, 2025
  • Usajili wa wafanyabiashara November 14, 2023
  • Tangazo la Uchaguzi wa Serikali za Mitaa 2024 August 15, 2024
  • Angalia zote

Habari Mpya

  • RAIS SAMIA AWAPUNGUZIA KODI WAFANYABIASHARA SOKO KUU LA KARIAKOO.

    March 09, 2026
  • DC MPOGOLO ATINGA KARIAKOO USIKU, BARABARA ZAFUNGUKA.

    March 09, 2026
  • KARIAKOO KUENDELEA KUWEKA MAZINGIRA WEZESHI KWA WANAWAKE

    March 05, 2026
  • KARIAKOO, URA SECURITY KUIMARISHA ULINZI SOKO LA KARIAKOO.

    February 27, 2026
  • Angalia zote

Video

Video zaidi

Viunganishi vya Haraka

  • TAMISEMI
  • eGovernment Authority
  • Employees Self Service Portal

Viunganishi Linganifu

World visitors tracker

world map hits counter

Wasiliana nasi

Other Contacts

   

Visitors Counter

www.freevisitorcounters.com

    • Maswali ya Mara kwa Mara
    • Sera ya faragha
    • Kanusho
    • Ramani ya tovuti
    • Huduma

Copyright ©2024 Shirika la Masoko ya Kariakoo . All rights reserved.