Na.OR-TAMISEMI
Naibu Waziri Ofisi ya Rais TAMISEMI, Mhe. Dkt. Festo Dugange amehimiza wananchi kujitokeza kupiga kura kuchagua viongozi wa Serikali za Mitaa kwa kuwa viongozi hao ndio wanaomsaidia Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kuleta maendeleo katika maeneo yao.
Mhe. Dugange ametoa kauli hiyo tarehe 4 Agosti, 2024 alipotembelea banda la Ofisi ya Rais TAMISEMI katika Maonesho ya Wakulima na Wafugaji (Nanenane) yanayofanyika katika Viwanja vya Nzuguni jijini Dodoma.
Pia, amewataka viongozi wa Mamlaka za Serikali za Mitaa kukitumia Chuo cha Serikali za Mitaa kutoa mafunzo kwa viongozi watakaochaguliwa katika uchaguzi wa Serikali za Mitaa unaotarajiwa kufanyika mwezi Oktoba 2024 na wale watakaochaguliwa katika Uchaguzi Mkuu utakaofanyika mwezi Oktoba 2025 ili waweze kutimiza majukumu yao ipasavyo.
General Manager, Kariakoo Markets Corporation, Nyamwezi/Tandamti Street,
Postal Address: P. O. Box 15789 Dar es Salaam, Tanzania
Telephone: +255 22 2180678
Mobile:
Email: info@kariakoomarket.co.tz
Copyright ©2024 Shirika la Masoko ya Kariakoo . All rights reserved.