Watumishi wa Shirika la Masoko ya Kariakoo wamekumbushwa kujitokeza na kujiandikisha kwenye Orodha ya Mpiga Kura wa Serikali za Mitaa kwa ajili ya kushiriki uchaguzi wa viongozi utakaofanyika Novemba 27 mwaka huu.
Wito huo umetolewa na Kaimu Meneja Mkuu wa Shirika la Masoko ya Kariakoo Mary Maridadi alipongea na Wakuu wa Idara na Vitengo kwenye kikao cha kawaida cha Menejimenti kilichofanyika ofisini kwake Magogoni jijini Dar es Salaam Oktoba 15, 2024 ambapo alisisitiza juu ya watumishi kwenda kujiandikisha kwenye daftari la wapiga kura ili watumie haki yao ya kidemokrasia kuchagua viongozi ngazi ya mitaa .
Zoezi la kujiandikishaji kwenye daftari la wapiga kura limeanza tarehe 11 hadi tarehe 20 Novemba mwaka huu ambapo kauli mbiu ya uchaguzi wa mkwa huu ni "Serikali za Mitaa, Sauti ya Wananchi, Jitokeze Kushiriki Uchaguzi".
General Manager, Kariakoo Markets Corporation, Nyamwezi/Tandamti Street,
Postal Address: P. O. Box 15789 Dar es Salaam, Tanzania
Telephone: +255 22 2180678
Mobile:
Email: info@kariakoomarket.co.tz
Copyright ©2024 Shirika la Masoko ya Kariakoo . All rights reserved.