Meneja Mkuu wa Shirika la Masoko Kariakoo Ashraph Abdulkrim ametanabaisha kuwa wamefanikiwa kuwafanyia uhakiki wafanyabiashara 1520 ambao waliafikiwa kwenye kamati ya Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam hatua inayopelekea kukamilsha hatua za awali kuelekea ufunguzi wa Soko la Kariakoo ambalo limekamilika kukarabatiwa na kujengwa upya
Alisema kuwa zoezi hilo limefanyika kwa uwazi na ukubwa wa kuridhisha hadi kufikia hatua ya kuwapangia na kuwarejesha kwenye maeneo yao tangu lilipokabidhiwa rasmi kwenye shirika baada ya ujenzi kukamilika.
Abdulkarim alisema alisema hayo 09 Oktoba 2025 wakati wa hafla ya kuadhimisha Wiki ya Huduma kwa Mteja iliyofanyika ndani ya Soko la Kariakoo na kuhudhuriwa na wafanyabiashara zaidi ya 200 ambapo amesisitiza kuwa wakati wanaendelea kuadhimisha wiki ya huduma kwa mteja wataendelea kulinda miundombinu ya jengo hilo kwa wivu mkubwa huku akitumia wiki hii kukutana na kutatua hoja na malalamiko yao ndani ya soko hilo.
Shirika la Masoko ya Kariakoo lipo kwenye maandalizi ya mwisho kuelekea kurejesha biashara ndani ya sok hilo ambapo Serikali ya Awamu ya Sita imelijenga kwa gharama ya shilingi Bilioni 28.03
General Manager, Kariakoo Markets Corporation, Nyamwezi/Tandamti Street,
Anuani ya posta: P. O. Box 15789 Dar es Salaam, Tanzania
Simu: +255 22 2180678
Simu ya kiganjani:
Baruapepe za Watumishi: info@kariakoomarket.co.tz
Copyright ©2024 Shirika la Masoko ya Kariakoo . All rights reserved.