Shirika la Masoko ya Kariakoo limechukua hatua muhimu kuelekea ufunguzi na urejeshaji wa biashara katika soko jipya la Kariakoo ambapo limetoa mafunzo kwa wafanyabiashara kuhusu mfumo wa kielektroniki wa TAUSI, udhibiti wa majanga, elimu ya bima, na fursa za mikopo ya biashara.
Kaimu Meneja Mkuu wa Shirika Mary Maridadi akifungua mafunzo hayo ya siku mbili (Machi 10,2025) Msimbazi, Dar es Salaam alisema lengo la mafunzo ni kuwawezesha wafanyabiashara kuelewa na kutumia mfumo wa kielektroniki wa TAUSI na pia kuandaa wafanyabiashara kwa ufunguzi wa soko na kurejesha biashara.
Akizungmza kuhusu Mfumo wa TAUSI Afisa TEHAMA wa Shirika Emmanuel Mjunguli alieleza kuwa mfumo huo ni mfumo rafiki unaowaruhusu wafanyabiashara kujisajili, kupata maeneo ya biashara, na kupata hati za malipo kwa urahisi.
Mjunguli aliongeza kusema wafanyabiashara wanaweza kujiunga na mfumo kupitia tovuti https://tausi.tamisemi.go.tz ambapo alitaja wanahitajika kuwa na namba ya kitambulisho cha Taifa na namba ya mlipa kodi (TIN).
Ramadhani Mtengule ni mfanyabiashara aliyeshiriki mafunzo hayo ambapo alionesha kufurahishwa na mafunzo hayo na kwamba yanatoa matumaini ya kurejea sokoni na kuendelea na biashara zao kwa tija.
Mafunzo yalihusisha watoa mada kutoka Mamlaka ya Mapato (TRA), Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (TAKUKURU), Benki za TCB na NBC, na Jeshi la Zimamoto na Uokoaji na yalilenga kuwafikia wafanyabiashara 1,520 watakaorejeshwa sokoni awamu ya kwanza.
Mwisho
General Manager, Kariakoo Markets Corporation, Nyamwezi/Tandamti Street,
Postal Address: P. O. Box 15789 Dar es Salaam, Tanzania
Telephone: +255 22 2180678
Mobile:
Email: info@kariakoomarket.co.tz
Copyright ©2024 Shirika la Masoko ya Kariakoo . All rights reserved.