Meneja Mkuu alieleza "Tumedhamiria kulifanya Soko kuwa la kimataifa kama maelekezo ya Mheshimiwa Raisi kwamba hapa ndio kitovu cha biashara kwa Dar es Salaam, ambapo Wafanyabiashara kutoka nje, na ndani ya Tanzania na mikoani wanakuja" aliendelea kueleza yakuwa "kwa sasa tunaweza kuongea kifua mbele kwamba tumefikia asilimia mia moja la soko letu la kariakoo kwamba ujenzi umekamilika. Kama unavyoweza kuona tulikuwa na matengenezo madogo ya fensi ambayo tayali yamefanyiwa kazi na kukamilika." Meneja huyo alisema hatua iliyofikia kwa sasa ni wataalamu wa shirika la Masoko wanafunzwa kuhusu matumizi na usimamizi wa mifumo mbalimbali iliyosimikwa kwenye Soko hilo, kwakuwa Soko limejengwa kwa ukubwa na mifumo mingi ya kisasa. Akiitaja baadhi ya mifumo hiyo ambayo ni mifumo ya kuzima moto, mifumo ya umeme, mifumo ya maji na mifumo ya TEHAMA.
General Manager, Kariakoo Markets Corporation, Nyamwezi/Tandamti Street,
Anuani ya posta: P. O. Box 15789 Dar es Salaam, Tanzania
Simu: +255 22 2180678
Simu ya kiganjani:
Baruapepe za Watumishi: info@kariakoomarket.co.tz
Copyright ©2024 Shirika la Masoko ya Kariakoo . All rights reserved.