SHIRIKA LA MASOKO KARIAKOO, OSHA WATETA KUELEKEA UFUNGUZI WA SOKO LA KARIAKOO.
Meneja Mkuu wa Shirika la Masoko ya Kariakoo CPA. Ashraph Abdulkarim amekutana na kufanya mazungumzo na Mtendaji Mkuu wa Wakala wa Usalama na Afya Mahali pa Kazi, mazungumzo ambayo yamejikita katika kuimarisha ushirikiano baina ya taasisi hizo mbili.
CPA. Abdulkarim amesema taasisi yake inalo jukumu la kuhakikisha wafanyabiashara na wafanyakazi wa soko la kariakoo kwa miundombinu yake kufanyiwa ukaguzi na kuthibitishwa na OSHA kuwa ni salama kwa matumizi na hivyo kuepuka athari zinazojitokeza.
“Mkurugenzi nimeona ni muhimu nije tufanye mazungumzo kabla soko halijafunguliwa, tuwaombe mfanye ukaguzi na kutushauri kitu cha kufanya ili tuweze kufanya kazi katika mazingira salama kwa manufaa ya shirika na watumiaji wa soko hilo” Amebainisha CPA. Abdulkarim
Kwa upande wake Mtendaji Mkuu wa OSHA, Khadija Mwenda amemhakikishia Meneja Mkuu wa Shirika la Masoko ya Kariakoo kuwa OSHA itafanya ukaguzi wa soko la Kariakoo haraka iwezekanavyo kutokana na umuhimu wa soko hilo katika kukuza uchumi wa nchi.
Ameongeza kuwa OSHA itahakikisha inatoa elimu kwa wafanyabiashara bure na kuweka utaratibu wa kusajili wafanyabiashara na kuwa na kamati za afya na usalama mahali pa kazi, kamati hizo zitaundwa na wafanyabiashara wenyewe na kuahidi baada ya wanyakazi hao kupatiwa elimu watapatiwa pia vifaa.
Copyright ©2024 Shirika la Masoko ya Kariakoo . All rights reserved.