Shirika la Masoko ya Kariakoo limeendesha mafunzo ya siku mbili kwa askari wanaotoa huduma za ulinzi wa soko hilo ikiwa ni mwendelezo wa maandalizi ya kufungua soko hilo la kimataifa tangu lilipofungwa mwaka 2021 kufuatia ajali ya moto.
Miongoni mwa mada zilizofundishwa katika mafunzo hayo ni pamoja na huduma bora kwa mteja pamoja na ukamataji salama na matumizi ya nguvu ya kadri wakati wa ukamataji pale watakapohitajika kufanya hivyo.
Akitoa mafunzo Mkaguzi wa Jeshi la Polisi Kata ya Kariakoo Afande Titus Kachira amewataka askari hao kutoa huduma zao kwa kutumia lugha nzuri na staha, kutoa msaada kwa wateja pale unapohitajika, kuwathamini wateja na kuepuka kutumia nguvu kubwa wakati wa ukamataji.
Afande Kachira ameongeza kuwa wateja watakaofika sokoni hapo wanaamini mahali watakapoweza kupata msaada wa haraka ni kwa askari waliopo katika eneo hilo na kubainisha kuwa endapo hawatapata huduma stahiki watakata tamaa na kwenda maeneo mengine ya huduma.
Akiongea kwa niaba ya Meneja Mkuu wa Shirika hilo, Mkuu wa Kitengo cha Usalama Bw. Jossam A. Mnzava amesema wameamua kutoa mafunzo hayo kwa askari hao kwa kutambua kuwa ni watu muhimu katika mnyororo wa utoaji wa huduma katika soko hilo.
Mafunzo hayo yaliyoanza Disemba 4 hadi 5, 2025 yametolewa kwa ushirikiano kati ya Shirika la Masoko ya Kariakoo na Jeshi la Polisi kwa uratibu wa Mkuu wa Ushirikishwaji Jamii Wilaya ya Kipolisi Kariakoo, Mrakibu wa Polisi Rosemary Kitwala.
General Manager, Kariakoo Markets Corporation, Nyamwezi/Tandamti Street,
Anuani ya posta: P. O. Box 15789 Dar es Salaam, Tanzania
Simu: +255 22 2180678
Simu ya kiganjani:
Baruapepe za Watumishi: info@kariakoomarket.co.tz
Copyright ©2024 Shirika la Masoko ya Kariakoo . All rights reserved.