• Wasiliana nasi |
    • Maswali ya Mara kwa Mara |
    • Complaints |
    • Gms |
SHIRIKA LA MASOKO YA KARIAKOO
SHIRIKA LA MASOKO YA KARIAKOO

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania OFISI YA RAIS TAWALA ZA MIKOA NA SERIKALI ZA MITAA SHIRIKA LA MASOKO YA KARIAKOO

  • Mwanzo
  • About KMC
    • Dira na Dhima
    • Muundo wa taasisi
    • Core Functions
  • Utawala
    • Idara
      • Human Resources and Administration
      • Health and Sanitation
      • Finance
      • Planning and Commercial
    • Vitengo
      • Maintenance Service
      • Internal Audit
      • Procurement Management
      • Information and Communication Technologies
      • Legal Services
      • Security
  • Kituo cha habari
    • Habari
    • Matangazo
    • Maktaba ya picha
    • Press-Releases
    • Video
  • Marketing
    • Products and Services
    • Marketing Price
  • Investment and Projects
    • Ongoing Projects
    • Miradi iliyokamilika
    • Upcoming Projects
    • Fursa za Uwekezaji
  • Manunuzi
    • Tenders
  • Machapisho
    • Miongozo
    • Fomu
    • Journals/Newsletter
    • Reports
    • Hotuba
  • E- Services Links
    • Revenue Collection(TAUSI)
    • GISP Portal
    • Employees Self Service Portal
    • E - Mrejesho
    • E - Board
    • E - Mikutano

CPA Abdulkarim: Soko la Kariakoo ni kwa Manufaa ya Wote

Posted on: July 29th, 2025

Wafanyabiashara wa Soko la Kariakoo wamehakikishiwa kuwa Serikali imejenga upya lililokuwa soko dogo na kukarabati soko lililoungua kwa ajili ya manufaa ya kiuchumi ya Watanzania wote bila ubaguzi.

Kauli hiyo imetolewa na Meneja Mkuu wa Shirika la Masoko ya Kariakoo CPA Ashraph Abdulkarim leo (28 Julai 2025) katika ukumbi wa soko la Machinga Dar es Salaam wakati alipofanya kikao na wafanyabiashara wa Soko hilo wanaotarajiwa kurejeshwa ndani ya soko.

CPA Abdulkarim alisema lengo la kikao hicho ni kuwapa mrejesho na taarifa juu ya maendeleo ya mradi na hatua zinazofanyika na Shirika kuwapanga wafanyabiashara ndani ya soko.

“Ninawaahidi kuwa tutasikiliza kila mfanyabiashara na kutatua changamoto zake kwa mujibu wa sheria na taratibu za upangishaji za Serikali ili kila mtu apate haki yake na kunufaika na uwepo wa soko la Kariakoo,” alisema CPA Abdulkarim.

Meneja Mkuu huyo amewasihi wafanyabiashara hao kuwa mabalozi wa soko hilo kwa kuelezea mazuri yanayofanywa na Serikali ili wananchi wanufaike.

Kikao hicho kilihusisha wafanyabiashara wa pembejeo, viuatilifu, mizani, cherehani, vifungashio, nafaka na viungo vikavu ambao wamepangiwa sakafu ya tatu, nne na tano soko jipya huku baadhi yao wakiwa na maoni ya kuboresha mchakato kuelekea ufunguzi wa soko hilo.

Emanuel Mbise, Mwenyekiti wa wauza pembejeo za kilimo alisema Shirika liweke wazi mikataba wa upangishaji pamoja na kutorusu biashara za pembejeo kuchanganywa na bidhaa zingine ili kulinda walaji.

Naye Abdala Bashiru Selemani alitoa rai kwa uongozi wa Shirika kuwapanga waliokuwa wafanyabiashara soko lililoungua ambao sasa watapangiwa soko jipya sakafu ya nne ili wawe na uhakiki wa biashara badala ya kuchanganywa na makundi mengine.

Ashraph Waziri mfanyabiashara ya nafaka aliomba Serikali ifikirie kuwapa muda wa matazamio na nafuu ya kodi wafanyabiashara wote ambao walipata hasara ya mali zao kutekeketea kwenye tukio la moto la 10 Julai 2021 kwa kuwa hakuna fidia yoyote hadi sasa waliopata.

Akijibu hoja na maswali hayo Meneja Mkuu CPA Abdulkarim alisema wataziratibu hoja hizo kuzitafutia majawabu ikiwemo kuongeza nafasi za majadiliano na wafanyabiashara wakati huu wa kuelekea ufunguzi wa Soko la Kariakoo ikiwemo kutoa elimu ya bima ya majanga ikiwemo moto.

Serikali ya Awamu ya Sita chini ya Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan ilitoa fedha shilingi Bilioni 28.03 ambazo zilifanya kazi ya kujenga soko jipya na kukarabati la zamani hatua inayofanya soko kuwa la kisasa ambapo maeneo ya biashara yameongezeka  toka 1,662 mwaka 2021 hadi 1,907 na ajira zaidi ya 4,000 zitazalishwa.

Mwisho

Matangazo

  • Taarifa kwa Umma January 31, 2025
  • Taarifa kwa Umma January 29, 2025
  • Usajili wa wafanyabiashara November 14, 2023
  • Tangazo la Uchaguzi wa Serikali za Mitaa 2024 August 15, 2024
  • Angalia zote

Habari Mpya

  • Maandalizi Ufunguzi wa Soko la Kariakoo Yakamilika

    October 11, 2025
  • Meneja Mkuu Shirika la Masoko Kariakoo, Bw. Ashiraf Abdulkarim anasema Kariakooo ndiyo Soko kubwa ambalo wafanyabiashara wa ndani na nje ya mipaka ya Tanzania wanakuja kufanya biashara.

    September 24, 2025
  • Dkt. Jafo: Wafanyabiashara Kariakoo Kuweni Mabalozi wa Amani

    August 15, 2025
  • Soko la Kariakoo Kuwa na Bima ya Majanga

    July 31, 2025
  • Angalia zote

Video

Video zaidi

Viunganishi vya Haraka

  • TAMISEMI
  • eGovernment Authority
  • Employees Self Service Portal

Viunganishi Linganifu

World visitors tracker

world map hits counter

Wasiliana nasi

    General Manager, Kariakoo Markets Corporation, Nyamwezi/Tandamti Street,

    Anuani ya posta: P. O. Box 15789 Dar es Salaam, Tanzania

    Simu: +255 22 2180678

    Simu ya kiganjani:

    Baruapepe za Watumishi: info@kariakoomarket.co.tz

Other Contacts

   

Visitors Counter

www.freevisitorcounters.com

    • Maswali ya Mara kwa Mara
    • Sera ya faragha
    • Kanusho
    • Ramani ya tovuti
    • Huduma

Copyright ©2024 Shirika la Masoko ya Kariakoo . All rights reserved.