Serikali ipo katika hatua za mwisho za kukamilisha taratibu za kuwarejesha wafanyabiashara kwenye Soko la Kariakoo kutokana na mradi wa ujenzi na ukarabati wa soko kufikia asilimia 93
Hatua kadhaa zimeendelea kuchukuliwa ikiwemo utambuzi na uhakiki wa waliokuwa wafanyabishara kabla ya janga la moto. Kazi nyingine inayoendelea ni kupanga biashara kulingana na eneo husika pamoja na kufuatilia madeni ya waliokuwa wafanyabiashara wa Soko la Kariakoo.
Akizungumza na waandishi wa habari Jijini Dar es Salaam (Aprili 22,2024) karibuni Kaimu Meneja Mkuu wa Shirika la Masoko ya Kariakoo Sigsibert Valentine alisema jumla ya Shilingi 497,773,019.26 zinadaiwa kwa waliokuwa wafanyabiashara ambapo zinatakiwa kulipwa kabla ya kurejea sokoni .
Valentine aliongeza kusema ni budi mdaiwa kulipa deni lake ili apate nafasi ya kusajiliwa na mfumo katika mfumo wa TAUSI vinginevyo atakuwa amepoteza sifa za kurejea sokoni.
Jitihada za Shirika la Masoko kufuatilia wafanyabiashara wanaodaiwa zinaendelea ambapo hadi sasa Shilingi 15,830,977.71 kimekusanywa hadi sasa aliongeza kusema Valentine.
"Nitoe wito kwa wafanyabiashara kuwa mfanyabiashara yeyote atakayeshindwa kutimiza wajibu wake wa kisheria wa kulipa deni alilokuwa amelimbikiza kabla ya kusitisha shughuli za biashara tarehe 10.07.2021 hatoweza kupata nafasi ya biashara kwenye soko jipya la Kariakoo" alisisitiza Valentine
Mwisho
General Manager, Kariakoo Markets Corporation, Nyamwezi/Tandamti Street,
Postal Address: P. O. Box 15789 Dar es Salaam, Tanzania
Telephone: +255 22 2180678
Mobile:
Email: info@kariakoomarket.co.tz
Copyright ©2024 Shirika la Masoko ya Kariakoo . All rights reserved.