Mwenyekiti wa Bodi ya Shirika la Masoko ya Kariakoo Hawa Ghasia amesema kuanzia Januari 31 mwaka huu kazi ya kupandisha kwenye mfumo majina ya wafanyabiashara 1,520 ambao walikuwepo kwenye soko la Kariakoo kabla ajali ya moto ya Julai 10,2021 itaanza.
Ametoa kauli hiyo jana (Januari 30,2025) wakati wa kikao cha Mkuu wa Mkoa wa Dare Salaam Albert Chalamila na waandishi wa habari kuhusu kutangaza kuwa ifikapo Februari 22 mwaka huu Soko la Kariakoo litaanza kufanya kazi saa Ishirini na Nne.
Ghasia aliongeza kuwa baada ya Shirika kupandisha majina kwenye mfumo, wafanyabiashara wanatakiwa kujaza fomu Maalum ili kuanza taratibu za kurejeshwa kwenye soko.
Katika hatua nyingine Mwenyekiti huyo alisema, hakuna mfanyabiashara ambaye atarejeshwa sokoni endapo hajalipa deni la awali na kubainisha kuwepo kwa wafanyabiashara 366 wanaodaiwa zaidi ya shilingi Milioni 358.Awali Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam Albert Chalamila alitangaza kuwa biashara kuwa biashara katika Jiji la Dar es Salaam zitafanyika kwa saa 24 kuanzia tarehe 22 Februari mwaka huu na kusisitiza kuwa maandalizi ikiwemo uwekaji taa katika maeneo ya Soko la Kariakoo ukiendelea vizuri
Soko la Kariakoo lilisitisha shughuli zake mwaka 2021 mara baada ya ajali ya moto ambapo kwa sasa serikali ya Awamu ya Sita imefanikisha kutumia shilingi Bilioni 28.03 kujenga na ukarabati lile la zamani.
Mwisho.
General Manager, Kariakoo Markets Corporation, Nyamwezi/Tandamti Street,
Postal Address: P. O. Box 15789 Dar es Salaam, Tanzania
Telephone: +255 22 2180678
Mobile:
Email: info@kariakoomarket.co.tz
Copyright ©2024 Shirika la Masoko ya Kariakoo . All rights reserved.