Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam Mhe Albert Chalamila amepokea taarifa ya kamati aliyoiunda kupitia orodha ya majina ya wafanyabiashara wa soko la Kariakoo katika ukumbi wa mikutano Arnatoglo Mnazi mmoja-Ilala Septemba 04,2024.
RC Chalamila akipokea taarifa hiyo amesema alilazimika kuunda kamati hiyo ili kujiridhisha juu ya mchakato mzima uliotumika kupata orodha ya majina ya awali ya wafanyabiashara hao kutokana na unyeti wa eneo la soko la Kariakoo kwa maslahi mapana ya Mkoa na Taifa kwa ujumla.
Aidha kikao hicho kilihudhuriwa na Mwenyekiti wa Bodi ya Shirika la Masoko Kariakoo Bi. Hawa Ghasia, Katibu Tawala wa Mkoa Dkt Toba Nguvila, Mkuu wa Wilaya ya Ilala Mhe Edward Mpogolo, Mkurugenzi wa Jiji Bwana Elihuruma Mabelya pamoja na wajumbe wa kamati wakiongozwa na Mwenyekiti Mhandisi Amani Mafuru.
Pamoja na masuala mengine Mkuu wa Mkoa Chalamila aliipongeza kamati hiyo kwa kazi nzuri na hatimaye baada ya kupokea ripoti hiyo alipata wasaa wa kupokea maoni na ushauri kutoka kwa wajumbe kwa lengo la kuwa na uelewa wa pamoja.
Mwisho.
General Manager, Kariakoo Markets Corporation, Nyamwezi/Tandamti Street,
Postal Address: P. O. Box 15789 Dar es Salaam, Tanzania
Telephone: +255 22 2180678
Mobile:
Email: info@kariakoomarket.co.tz
Copyright ©2024 Shirika la Masoko ya Kariakoo . All rights reserved.