• Wasiliana nasi |
    • Maswali ya Mara kwa Mara |
    • Complaints |
    • Gms |
SHIRIKA LA MASOKO YA KARIAKOO
SHIRIKA LA MASOKO YA KARIAKOO

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania OFISI YA RAIS TAWALA ZA MIKOA NA SERIKALI ZA MITAA SHIRIKA LA MASOKO YA KARIAKOO

  • Mwanzo
  • Kuhusu sisi
    • Dira na Dhima
    • Muundo wa Taasisi
    • Majukumu ya msingi
  • Utawala
    • Idara
      • Human Resources and Administration
      • Health and Sanitation
      • Finance
      • Planning and Commercial
    • Vitengo
      • Maintenance Service
      • Internal Audit
      • Procurement Management
      • Information and Communication Technologies
      • Legal Services
      • Security
  • Kituo cha habari
    • Habari
    • Matangazo
    • Maktaba ya picha
    • Press-Releases
    • Video
  • Marketing
    • Products and Services
    • Marketing Price
  • Miradi na Fursa za uwekezaji
    • Miradi iliyokamilika
    • Miradi inayoendelea
    • Miradi itakayotekelezwa
    • Fursa za Uwekezaji
  • Manunuzi
    • Zabuni
  • Machapisho
    • Miongozo
    • Fomu
    • Journals/Newsletter
    • Reports
    • Hotuba
  • Huduma mtandao
    • Revenue Collection(TAUSI)
    • GISP Portal
    • Employees Self Service Portal
    • E - Mrejesho
    • E - Board
    • E - Mikutano

SHIRIKA LA MASOKO YA KARIAKOO LAANZA KUANDAA MPANGO MKAKATI WA MIAKA MITANO 2026-2031.

Posted on: December 12th, 2025

SHIRIKA LA MASOKO YA KARIAKOO LAANZA KUANDAA MPANGO MKAKATI WA MIAKA MITANO 2026-2031.


Shirika la Masoko ya Kariakoo limeanza rasmi maandalizi ya Mpango Mkakati mpya wa miaka mitano 2026-2031, hatua inayolenga kulifanya soko hilo la kimataifa kutoa huduma bora, kwa wakati na kuzingatia mabadiliko ya teknolojia yanayojitokeza duniani.


Mpango huo unakuja baada ya mpango wa mwaka 2021-2025 kumaliza muda wake wa utekelezaji kwa mafanikio makubwa.


Akizungumza wakati wa ufunguzi mafunzo ya uchambuzi na uandaaji wa mpango huo, Meneja Mkuu wa Shirika la Masoko ya Kariakoo, CPA. Ashiraf Abdulkarim , amesema maandalizi ya mpango huo umeshirikisha wadau ikiwemo Ofisi Waziri Mkuu TAMISEMI, Wafanyabiashara wa Kariakoo, Wapangaji na wadau wengine  ili kuwa na mpango mkakati bora, uliochukua mawazo ya wengi na unaojibu matamanio ya kila mmoja na hivyo kuwa rahisi katika utekelezaji wake.


CPA Abdulkarim ameongeza kuwa  katika kuandaa mpango huo, Shirika litazingatia nyaraka mbalimbali ikiwemo Dira ya Maendeleo ya  Taifa 2025-2050, hotuba ya Rais wakati akifungua Bunge la 13, Mpango wa Nne wa Maendeleo wa Taifa, Ilani ya Uchaguzi ya mwaka 2025-2030 pamoja na Sheria na miongozo mbalimbali iliyoanzisha Shirika la Kariakoo.


“Mafunzo haya yatafanyika kwa siku tano na yatakuwa endelevu. Lengo ni kuwa na mpango mkakati bora, unaotekelezeka na unaoweza kupimika kila mwaka kwa kipindi cha miaka mitano ambao utalifanya soko la kariakoo kuwa kinara na linalotoa huduma anuai na sio mazao pekee" amebainisha CPA Abdulkarim.


Amesema  mpango huo ukikamilika utalibadilisha soko la Kariakoo kuwa kituo cha kisasa cha biashara, chenye mifumo ya kisasa ya uendeshaji na utoaji huduma.


CPA. Abdulkarim amesema kuwa Kariakoo mpya itakuwa na miundombinu ya kisasa kuanzia maeneo ya maegesho ya magari, mifumo ya kuzima moto, maeneo ya dharura, hewa ya kutosha na mifumo ya kiteknolojia ya uendeshaji. Tunataka kuwahudumia Watanzania katika mazingira bora na ya kisasa.


Kwa upande wake, Meneja wa Mipango na Biashara wa Shirika la Kariakoo, Bi. Mwinga Luhoyo amesema maandalizi ya mpango huo yanahusisha tathmini ya mpango uliopita wa 2021–2025 ili kubaini mafanikio, changamoto na maeneo yanayohitaji maboresho.


Meneja huyo ameongeza kuwa lengo ni kuhakikisha mpango huo unaendana na mikakati ya kitaifa na huku ukilenga kuongeza tija, kuimarisha biashara, na kukuza mchango wa Kariakoo katika uchumi wa taifa.

Matangazo

  • Taarifa kwa Umma January 31, 2025
  • Taarifa kwa Umma January 29, 2025
  • Usajili wa wafanyabiashara November 14, 2023
  • Tangazo la Uchaguzi wa Serikali za Mitaa 2024 August 15, 2024
  • Angalia zote

Habari Mpya

  • SOKO LA KARIAKOO MBIONI KUFUNGULIWA

    December 19, 2025
  • SHIRIKA LA MASOKO YA KARIAKOO LAANZA KUANDAA MPANGO MKAKATI WA MIAKA MITANO 2026-2031.

    December 12, 2025
  • ASKARI WA SHIRIKA LA MASOKO KARIAKOO WANOLEWA KUHUSU HUDUDUMA BORA KWA MTEJA.

    December 05, 2025
  • ASKARI WA SHIRIKA LA MASOKO KARIAKOO WANOLEWA KUHUSU HUDUDUMA BORA KWA MTEJA.

    December 05, 2025
  • Angalia zote

Video

Video zaidi

Viunganishi vya Haraka

  • TAMISEMI
  • eGovernment Authority
  • Employees Self Service Portal

Viunganishi Linganifu

World visitors tracker

world map hits counter

Wasiliana nasi

    General Manager, Kariakoo Markets Corporation, Nyamwezi/Tandamti Street,

    Anuani ya posta: P. O. Box 15789 Dar es Salaam, Tanzania

    Simu: +255 22 2180678

    Simu ya kiganjani:

    Baruapepe za Watumishi: info@kariakoomarket.co.tz

Other Contacts

   

Visitors Counter

www.freevisitorcounters.com

    • Maswali ya Mara kwa Mara
    • Sera ya faragha
    • Kanusho
    • Ramani ya tovuti
    • Huduma

Copyright ©2024 Shirika la Masoko ya Kariakoo . All rights reserved.