Shirika la Masoko ya Kariakoo limepata Meneja Mkuu mpya CPA Ashraph Yusuph Abdulkarim.
Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa na Kurugenzi ya Mawasiliano ya Rais,Ikulu (25 Machi,2025) imesema Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan amemteua CPA Abdulkarim kuwa Meneja Mkuu wa Shirika la Masoko ya Kariakoo.
Shirika la Masoko ya Kariakoo lilianzishwa mwaka 1974 ambapo majukumu yake makuu ni kusimamia na kuendesha soko kuu la Kariakoo pamoja na masoko mengine yatakayoanzishwa chini yake ,kujenga masoko mengine mapya katika mkoa wa Dar es Salaam na kutoza ushuru au kodi aina yoyote ya soko lililo chini yake.
Kwa sasa Soko la Kariakoo liko katika hatua ya kurejesha biashara pamoja na wafanyabiashara kufuatia kukamilika kwa mradi mkubwa wa kimkakati wa ujenzi wa soko jipya na ukarabati wa soko kuu la zamani uliofanywa na Serikali ya Awamu ya Sita kuanzia mwaka 2022 ambapo umekamilika kwa gharama za shilingi Bilioni 28.03.
Shughuli za kuwarejesha na kuwapangia maeneo ya biashara ndani ya Soko zinaendelea ambapo Mfumo wa TAUSI unatumika huku soko likitarajiwa kuanza kazi mwezi Aprili mwaka huu na kwamba jumla ya wafanyabiashara zaidi ya 2000 wataingia sokoni.
General Manager, Kariakoo Markets Corporation, Nyamwezi/Tandamti Street,
Postal Address: P. O. Box 15789 Dar es Salaam, Tanzania
Telephone: +255 22 2180678
Mobile:
Email: info@kariakoomarket.co.tz
Copyright ©2024 Shirika la Masoko ya Kariakoo . All rights reserved.