Shirika la Masoko ya Kariakoo linatarajiwa kuanza kufanya biashara kwa muda wa masaa ishinini na nne kuanzia mwezi Februari mwaka huu baada ya kazi ya ujenzi na ukarabati kukamilika.
Katika kuhahikisha kuwa Shirika linaimarisha mapato yake na kuondoa madeni ya awali , kigezo cha wenye madeni kuhakikisha wanalipa kabla ya kurejea sokoni Kariakoo kimewekwa . Orodha ya wafanyabiashara itapandishwa kwenye mfumo mwisho mwa wiki hii kuwezesha wananchi kuona majina yao yaliyokidhi vigezo na sifa za uhakiki.
Akizungumza na waandishi wa habari (Januari 29,2025) Dar es Salaam , Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi wa Shirika hilo, Mhe. Hawa Ghasia alisema hakutakuwa na mfanyabiashara mwenye deni atakayerejeshwa sokoni hivyo akatoa wito kwa Wafanyabiashara wote wenye madeni kulipa madeni yao kabla ya kurejea Sokoni.
"Takwimu zetu zinaonyesha jumla ya wafanyabiashara 366 wanadaiwa na Shirika Shilingi 358,571,106.85. Deni hili lilikuwepo tangu kabla ya ajali ya moto ya tarehe 10 Julai 2021" alisisitiza Mhe. Ghasia.
Katika hatua nyingine, Mwenyekiti huyo wa Bodi amemshukuru Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt.Samia Suluhu Hassan kwa kutoa fedha shilingi BILIONI 28.03 zilizofanikisha ujenzi na ukarabati wa soko la Kariakoo.
General Manager, Kariakoo Markets Corporation, Nyamwezi/Tandamti Street,
Postal Address: P. O. Box 15789 Dar es Salaam, Tanzania
Telephone: +255 22 2180678
Mobile:
Email: info@kariakoomarket.co.tz
Copyright ©2024 Shirika la Masoko ya Kariakoo . All rights reserved.