Shirika la Masoko ya Kariakoo linaendelea na taratibu za maandalizi ya kurejesha shughuli za biashara katika Soko la Kariakoo kufuatia kutangazwa kwa majina ya wafanyabiashara wenye sifa za kurejeshwa sokoni ambapo kazi ya usajili wa wafanyabiashara inaendelea.
Katika utekelezaji wa wa mpango wa urejeshwaji shuguguli katika soko la Kariakoo, Shirika linaratibu kutoaji wa fomu maalum za usajili ambapo hadi kufikia leo (Februari 06,2025) jumla ya wafanyabiashara 1,094 kati ya 1,520 tayari wamechukua fomu katika ukumbi wa mikutano wa Arnautoglo Dar es Salaam kuchukua fomu maalum za usajili .Aidha, kati ya waliochukua fomu 707 tayari wamejaza na kurejesha fomu zao
Kwa mujibu wa ratiba iliyotolewa na Menejimenti ya Shirika la Masoko ya Kariakoo imeonesha kuwa ya ya kuchukua kuchukua, kujaza na kisha kurejesha fomu hizo ilianza tarehe 3 mwezi huu na itakamilika siku ya Ijumaa tarehe 7 Februari 2025 kisha taratibu za utayarishaji kanzi data kwenye mfumo wa TAUSI kabla ya kuingia mikataba kati ya Shirika na mfanyabiashara itaendelea.
Wito unatolewa kwa wafanyabiashara wote ambao majina yao yametangazwa kutumia muda uliotolewa ili kuchukua na kujaza fomu hizo maalum hatua itakayosaidia kurahishisha utartibu wa kurejesha biashara kwenye soko la Kariakoo.
Itakumbukwa kuwa Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi wa Shirika la Masoko ya Kariakoo hawa Ghasia alitangaza mwishoni mwa wiki iliyopita kuwa biashara katika Soko la Kariakoo zitarejeshwa tena kuanzia mwezi huu na kwamba ifikapo Februari 22 mwaka huu zitaanza kufanyika kwa muda wa saa 24.--
General Manager, Kariakoo Markets Corporation, Nyamwezi/Tandamti Street,
Postal Address: P. O. Box 15789 Dar es Salaam, Tanzania
Telephone: +255 22 2180678
Mobile:
Email: info@kariakoomarket.co.tz
Copyright ©2024 Shirika la Masoko ya Kariakoo . All rights reserved.