Click here to open the Project document
Miradi ya Maendeleo iliyotekelezwa na Uwekezaji
Shirika la Masoko ya Kariakoo kama ilivyo kwa taasisi nyingine za serikali linayo mipango madhubuti ya Uwekezaji kwa ajili ya maendeleo yake. Katika kipindi chote ambapo limekuwepo kutekeleza shughuli zake kwa mujibu wa Sheria yake, limefanikiwa kutekeleza shughuli kadhaa za kimaendeleo. Miongoni mwa shughuli hizo ni kama vile;
Usimamizi wa Soko Kuu na Soko Dogo kwamba Masoko haya yote yameendelea kuwepo tangu yalipojengwa na kuanza kutumika katika uingizaji wa mapato.
Shirika limefanikiwa kujenga nyumba saba (7) za kawaida na Ghorofa moja katika maeneo ya Mbezi Beach- Makonde na Tabata Bima.
Shirika limenunua rasilimali ardhi (Viwanja) na kumiliki katika maeneo ya Mbezi Beach Makonde na Tabata Bima, kwa ajili ya kufanya uwekezaji.Ukubwa wa maeneo yote kwa pamoja ni hekta
Shirika lina eneo la Soko Dogo ambalo linahitaji Uwekezaji mkubwa kwa kujenga Jengo jipya la Kisasa ambalo litaweza kutoa nafasi nyingi za maeneo ya kufanya biashara, Maegesho ya magari na huduma nyingine za kibiashara. Eneo hili lina eneo lina Mita za Mraba 3598. Mbezi Beach Makonde kuna Mita za Mraba 6119 na Tabata Bima ni mita za mraba 10117.14. Hatua za awali zimeanza kwa ajili ya kupata Wawekezaji kupitia njia mbalimbali za kiuwekezaji.
General Manager, Kariakoo Markets Corporation, Nyamwezi/Tandamti Street,
Postal Address: P. O. Box 15789 Dar es Salaam, Tanzania
Telephone: +255 22 2180678
Mobile:
Email: info@kariakoomarket.co.tz
Copyright ©2024 Shirika la Masoko ya Kariakoo . All rights reserved.